FAHAMU YA NDOA KABLA YA NDOA

Sh6,000

Category:

Description

Mapenzi kabla ya ndoa huwezi kuyakuta ndani ya ndoa. Ndani ya ndoa utakutana na mambo tofauti kabisa. Tena mengine ni ya ajabu kweli. Unajua kwa nini? Mapenzi kabla ya ndoa yamejaa maigizo, mapenzi ndani ya ndoa yamejaa uhalisia. Hauwezi kuupata uhalisia wa mwenzako kabla ya ndoa kwa hiyo habari za kusema bado tunasomana hazisaidii maana mnasomana kwenye maigizo.

Ndani ya ndoa unaweza kabisa usikutane na lugha ya “I love you sweetheart” na lugha nyingine zenye ladha tamu. Badala yake ukakutana na lugha za maudhi na kero kwa wingi. Usishangae kabisa yule uliyempenda kabla ya ndoa ni mlevi, mzinzi, mwizi, muongo, mchonganishi, mlafi, mgomvi, mdangaji kupindukia na wakati kabla ya ndoa alikwambia anapenda kwaya. Kwahiyo nimekuandikia kitabu hiki cha Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa kukushirikisha mengi kuhusu ndoa ili ukiamua kuingia basi utakayoyakuta huko yasikuvunje moyo ukavunja mtu maana vijana wa siku hizi hamna vifua kabisa.Kitu kidogo tu mnauana.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “FAHAMU YA NDOA KABLA YA NDOA”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

General Inquiries

There are no inquiries yet.

You may also like…